Your Health Is Our Priority

Your Health Is Our Priority

Fahamu umuhimu wa vyakula mbalimbali

Jua vyakula na mimea tiba maalumu kwa ajili ya afya bora kwako na kwa familia yako

Dondoo za ndoa Bora na yenye Furaha

Fahamu jinsi ya kuimarisha na kuijenga Ndoa yako iwe imara na ya mda mrefu

Dondoo za Mazoezi yatakayo kukinga na Magonjwa mbalimbali

Fahamu mazoezi bora na yenye manufaa yatakayo kuweka vizuri na kukinga na Magonjwa Mbalimbali

Dondoo za Malezi Bora ya Mtoto

Fahamu saikolojia ya watoto,malezi bora na vitu wavitakavyo kwa ajili ya ukuaji mzuri na furaha

Fahamu MbogaMboga na matunda ambayo ni muhimu sana kwa afya yako

Pata taarifa juu ya mbogamboga na matunda,misimu yake pamoja na faida zake

Friday, August 12, 2016

Kutizama Tv kunaweza kukuua, utafiti

Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Japan umethibitisha kwamba kukaa kwa mda mrefu na kutazama vipindi vya televisheni kwa masaa mengi kunahatarisha afya kwani huhusishwa na maradhi yanasababisha mzunguko wa damu mwilini kutokuwa sawa.
Watafiti hao wanasema, hali hiyo pia huenda ikasababisha damu kuganda na kutengeneza vidonge katika sehemu kama vile miguu, na iwapo mgando huo utasukumwa na nguvu za mzunguko wa damu na kuingia sehemu kama vile mapafu, husababisha vifo.
Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku.
Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miaka 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990.
Matokeo yalikuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama televisheni, nayo hatari ya kupata ugonjwa huo wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40%.

Iligundulika pia kuwa waliotazama vipindi vya televisheni kwa zaidi ya saa 5 walikuwa katika hatari zaidi kuliko waliotazama televisheni kwa mda wa chini ya saa 3.
Zaidi ya hayo watu huambatanisha kitendo cha kukaa na kutazama televisheni huku wakila vitafunio kama vile Popcorns na Crisps ambavyo pia huwasababishia si tu mwili kukosa mazoezi bali pia kuongezeka kwa uzito unaohatarisha afya.

Monday, April 25, 2016

Atumia vidonge vya nguvu za kiume kuzoa kura

Katika mataifa mengi ya Afrika wakati wa uchaguzi wanasiasa hutoa pesa ilikuwashawishi wapigaji kura kuwachagua.
Lakini huko Korea Kusini amini usiamini, polisi wameanzisha uchunguzi baada ya kuibuka madai kuwa wapiga kura wenye umri wa makamo walimpigia mwanasiasa fulani eti kwa sababu aliwapa vidonge vya kuongeza nguvu za kiume!
Yamkini mwanasiasa mmoja aliwashawishi watu hao wenye umri wa makaomo kwa kuwapa vidonge.
Mbunge wa eneo hilo la Suwon iliyoko karibu na mji mkuu wa Seoul ndiye anayetuhumiwa kwa njama hiyo.
Suwon ilishuhudia upinzani mkali katika uchaguzi uliofanyika Jumatano iliyopita
jina la mshukiwa mkuu halijatajwa hadi ushahidi utakapopatikana.Hata hivyo uchunguzi wa msingi umethibitisha kuwa mgombea huyo alikuwa na kiwango kikubwa mno cha madawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa wakati mmoja.
Haijabainika ni kwanini wala alikusudia kuwapa kina nani.
Uchunguzi bado unaendelea.

Thursday, October 22, 2015

Saratani:Watu warefu wamo hatarini




Utafiti wa kampuni moja ya Sweden uliofanyiwa watu milioni 5 umeonekana kuthibitisha nadharia kwamba urefu wa mtu na hatari za ugonjwa wa saratani zina uhusiano.
Utafiti huo umebaini kwamba watu warefu wana hatari ya kushikwa na saratani ya matiti pamoja na ile ya gozi miongoni kwa magonjwa kadhaa ya saratani.
Matokeo yake yalibaini kwamba kwa kila ziada ya sentimita 10,wakati mtu anapokuwa mtu mzima hatari za kushikwa na saratani huongezeka kwa asilimia 18 miongoni mwa wanawake na asilimia 11 miongoni mwa wanaume.



Lakini wataalam walisema kuwa utafiti huo haukuangazia hatari nyingine ambazo watu warefu hawafai kuwa na wasiwasi nazo.
Tafiti za awali zimeonyesha uhusiano kati ya urefu wa mwanadamu na hatari za kushikwa na ugonjwa wa saratani,ijapokuwa haijulikani ni kwa nini.
Ripoti za awali za utafiti huo zilizowasilishwa katika mkutano wa wagonjwa wa watoto,watafiti kutoka taasisi ya Karolinska mjini Stockholm walielezea vile walivyolifuatilia kundi moja la watu wazima kwa zaidi ya miaka 50.


 Wanawake warefu wana hatari kubwa ya hadi asilimia 20 ya kupatikana na saratani ya matiti huku wanaume na wanawake warefu wakiwa na hatari ya juu ya kupatikana na saratani ya ngozi kwa asilimia 30


Daktari bandia aliwaambukiza Ukimwi watu 100

Mwanaume mmoja aliyejidai kuwa daktari na kuwaambukiza watu zaidi ya mia moja virusi amefikishwa mahakamani nchini Cambodia.
Yamkini daktari huyo bandia alikuwa akiwadunga wagonjwa wake kwa sindano aliyokuwa ameitumia kwa mgonjwa aliyekuwa na virusi vya Ukimwi.
Yem Chhrin anakabiliwa na kosa la kuua na kuambukiza watu ugonjwa huo kwa kukusudia.
Aidha Bw Yem anashtakiwa kwa kuwalaghai watu kuwa ni daktari ilhali hana vyeti halali vya kuhudumia umma.
Iwapo atapatikana na hatia mahakama ya nchi hiyo huenda ikamhukumu kifungo cha maisha jela.

Waathiriwa walioambukizwa maradhi ya Ukimwi wanatokea katika kijiji cha Roka kilichoko Kaskazini Magharibi.
Mmoja wao ni kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Buddha na mtoto wa miaka mitatu.
Takriban 10 kati ya waathiriwa hao wanakisiwa kuwa wameshakata roho.
Kwa mujibu wa ripoti za mahakama daktari huyo bandia amekiri kuhudumu bila vyeti maalum ila anakana kukusudia kuwaambukiza watu hao 100 virusi vinavyosababisha maradhi ya Ukimwi.

Sunday, October 18, 2015

Utafiti: Pilipili huchangia maisha marefu

Kwa miaka mingi sasa, binadamu amekuwa akitumia pilipili kuongeza ladha kwenye mlo wake. Kuna wanaovutiwa na ukali wake na vilevile wanaoichukia kutokana na ukali huo.
Sasa utafiti umeonyesha si ladha tu ambayo pilipili huongeza, bali pia hufanya wanaoila kuwa na maisha marefu.
Matokeo ya utafiti yaliyochapishwa kwenye jarida moja la matibabu nchini Uingereza kwa jina British Medical Journal yanasema kula mlo uliotiwa viungo, ikiwemo pilipili, huwa na manufaa kwa afya ya binadamu.
Wanasayanasi kutoka Uchina waliangazia afya ya watu takriban laki tano waliojitolea kushirikishwa katika utafiti kuhusu manufaa ya pipili kwa muda wa miaka kadhaa.
Matokeo ya uchunguzi huo yamebaini kuwa wahusika waliokula chakula kilichokuwa na wingi wa viungo, mara moja ama mara mbili kwa wiki walipunguza hatari yao ya kufa kwa asilimia 10.
Viwango vya hatari ya kufariki pia vilionekana kupungua kwa kiasi kikubwa kwa waliokula vyakula vilivyotiwa vikolezo kwa wingi kila siku.
Katika uchunguzi huo, sehemu kubwa ya viungo kwenye chakula ilikuwa pilipili, na kwa waliokula pipili mbichi walionekana kupunguza hatari ya kufariki kutokana na saratani, ugonjwa wa kisukari na pia maradhi ya moyo.
Mmoja wa walioongoza utafiti huo, Lu Qi,anayesema anapenda sana vyakula vyenye viungo vikali anasema kuna sababu nyingi za manufaa hayo.
"Takwimu hizi zinaonyesha watu wanafaa kula vyakula vyenye viungo Zaidi ili kuboresha afya yao na kupunguza hatari ya kufariki dunia wakiwa wachanga,” alisema Qi, ambaye ni mtaaamu wa lishe katika kitivo cha afya ya umma katika Chuo Kikuu cha Harvard.
Hata hivyo, anatahadharisha kwamba vyakula vyenye viungo vikali haviwezi kuwafaa watu wenye matatizo ya tumboni kama vile vindonda vya tumbo.

Faida 5 Kubwa Za Machungwa

1.Machungwa hupunguza Shinikizo la damu.
Virutubisho (Phytonutrients) vitwavyo herperidin’s vipatikanavyo katika machungwa  vinasaidia kupunguza shinikizo la damu.Pia tunda hili jamii ya citrus lina kiasi kikubwa cha folate ambayo husaidia kupunguza uwezekano wa kupata cardiovascular deseases(Magonjwa  ya moyo).


2.Hupunguza Lehemu(Cholestrol) kwa kiasi kikubwa.
Limonin ambayo hupatikana katika machungwa husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza cholestrol katika mwili wa binaadamu.

3.Huzuia Magonjwa ya Figo.
Machungwa husaidia kuzuia mawe katika figo(Kidney Stones) na husaidia figo kuchuja sumu ziingiazo mwilini ipasavyo.Kunywa 1/2 mpaka  Lita 1 ya juisi ya machungwa kwa siku itasaidia kupunguza kiasi cha pH  katika mkojo kitu ambacho kitapunguza uwezekano wa kutengenezwa mawe(Kidney stones) katika figo.

4.Hupunguza uwezekano wa kupata Ulcers(Vidonda vya tumbo)
Je umechoka kupata Ulcers?au unataka usipate? Basi tunda la chungwa ndio mkombozi wako.Kiasi kikubwa cha vitamin C kipatikanacho katika chungwa kinasaidia kuulinda mwili kutokana na Helicobacter pylori(H.pylori) bacteria ambae husababisha peptic Ulcers(Vidonda  vya tumbo).Vidonda  vya tumbo vikijirudia mara kwa mara humsababishia mgonjwa kupata kansa ya tumbo baadae katika maisha hivyo jilinde kwa kuhakikisha unakunywa japo glasi moja tu ya juisi ya machungwa kwa siku.

5.Kinga ya Mwili(Immune Support)
Tunda la chungwa lina kiasi kikubwa cha vitamin C ambayo huukinga  mwili kutokana na bacteria na virusi.Vitamin C ni muhimu kwa kusaidia kuharibika kwa celi (preventing cell damage) kwa kuondoa free radicals na kulinda DNA (Cancer prevention).Pia VitaminC inasaidia mfumo wa kinga ya mwili na husaidia kuzuia mafua na infections katika  masikio.



Umuhimu wa Mboga za Majani

Watu wanaokula mboga za majani katika milo yao ya kila siku wana faida kubwa ya kujikinga na magonjwa mbalimbali  sababu mboga za  majani zina madini na virutubisho  vya kutosha ambavyo upungufu wake humpelekea mtu kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa mbalimbali kutokana na upungufu na ukosefu wa madini linzi na virutubisho linzi katika mwili